Niyonzima |
Na Arone Mpanduka
Siku chache baada ya kuvunjiwa mkataba wake na klabu
ya Yanga, kiungo Haruna Niyonzima amesema hadi sasa hajapata barua rasmi ya
uamuzi huo.
Disemba 28 mwaka jana, Yanga ilitangaza kuvunja
mkataba wa kiungo huyo kwa madai kwamba alikiuka baadhi ya masharti ya mkataba.
Yanga ilisema ilimpa muda wa kuandaa na kuwasilisha
maelezo yake lakini Niyonzima hakutekeleza agizo hilo.
Akizungumza na kipindi cha michezo cha Kutoka Viwanjani
cha Redio Tumaini, Niyonzima alisema haelewi kitu kinachofanya Yanga kushindwa
kumpa barua yake hadi sasa.
Alisema jambo hilo linamfanya atambulike kama
mchezaji halali wa Yanga.
“Ninashindwa kuelewa nini kimetokea hadi barua yangu
nashindwa kuipata hadi sasa.Haina tabu, nitaendelea kusubiri hadi watakaponipa”
Kilichomponza Hartuna hadi kusimamishwa hivi
karibuni ni kitendo cha kuchelewa kujiunga na timu hiyo baada ya kwenda nchini
Ethiopia kushiriki mashindano ya Chalenji akiwa na timu yake ya taifa ya
Rwanda.
0 comments:
Post a Comment