CHEKA:"WATANZANIA NJOONI LEADERS"

Bondia Francis Cheka amewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kwenye pambano lake la leo la kusaka ubingwa wa dunia wa WBF dhidi ya Mserbia Gerard Ajetovic kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam.

Hapo jana mabondia hao walipima uzito ambapo kila mmoja alifanikiwa kuwa na kilogramu 72 zinazokubalika kisheria katika pambano lao.

Cheka alizidi kilogramu 2 lakini alitakiwa kupunguza uzito ndani ya saa mbili, zoezi ambalo alilifanikisha baada ya kukimbia na kuruka kichurachura.

Kupitia ukurasa wake wa facebook,Cheka amewaomba wapenzi wa masumbwi kufurika kwa wingi ili kumpa sapoti.

Pambano hilo litaanza majira ya usiku baada ya kumalizika kwa mapambano ya utangulizi yatakayoanza saa 12 jioni.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment