TWIGA STARS IKISHINDA KILA MCHEZAJI ATALAMBA 300,000




Naibu Waziri wa habari,Utamaduni,Wasanii na Michezo Anastazia Wambura leo ameitembelea kambi ya timu ya Taifa ya soka la wanawake Twiga Stars na kuahidi kutoa motisha ya shilingi laki tatu kwa kila mchezaji endapo wataifunga Zimbabwe siku ya Machi 5 mwaka huu.

Mchezo huo wa kuania kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika kwa wanawake kati ya Twiga na Zimbabwe utachezwa kuanzia saa 10 jioni kwewnye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Wakati akizungumza na timu hiyo Naibu Waziri Anastazia amehaidi kila mchezaji kupata shilingi 300,000 endapo watashinda katika mchezo huo.

Amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau wa michezo wamekusanya shilingi milioni 15 ambazo zitatumika kama motisha kwa wachezaji hao.

Waziri Anastazia amesema ni kweli timu hiyo haina wadhamini lakini wao kama Serikali wamepokea fedha hizo kutoka kwa wadau mbalimbali wa soka na watazigawa kwa wachezaji hao endapo wataifunga timu hiyo katika mchezo wao wa kwanza na katika mchezo wao wa marudiano utakaochezwa nchini Zimbabwe.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment