TFF YAMPONGEZA RAIS MPYA FIFA

Shirikisho la soka nchini TFF limempongeza rais mpya wa Shirikisho la soka duniani FIFA,Gianni Infantino kufuatia ushindi aliopata usiku wa jana.

Rais wa TFF Jamal Malinzi ametoa pongezi hizo kupitia ukurasa wake wa twitter.

Infantino anachukua nafasi ya Sepp Blatter aliyetangaza kujiuzulu miezi kadhaa iliyopita kufuatia kuandamwa na kashfa ya rushwa.

Blatter alikuwa kama ameota mizizi FIFA kufuatia kuiongoza tangu mwaka 1998.

Wajumbe kutoka mataifa 207 yanayotambuliwa na Fifa duniani walishiriki uchaguzi huo mjini Zurich kuamua mrithi wa Sepp Blatter.

Kabla ya upigaji kura kuanza, mageuzi kadha yalipitishwa, lengo likiwa kufanya Fifa kuwa na uwazi na uwajibikaji zaidi.

Kufuatia mabadiliko hayo, mishahara yote ya maafisa wa Fifa inafaa kuwekwa wazi siku za usoni.

Kutakuwa pia na kipimo kwenye muhula wa urais.

Baraza jipya pia litaundwa kuchukua nafasi ya kamati kuu tendaji, ambalo litakuwa na mwakilishi mwanamke kutoka kila shirikisho.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment