Na Arone Mpanduka
Mwanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini TASWA, Fred Mosha amefariki dunia.
Fred Mosha ambaye ni mmoja wa waasisi wa vipindi vya michezo vya Redio Tumaini amefariki kwenye hospitali ya Muhimbili alfajiri ya leo baada ya kuugua saratani ya shingo kwa muda mfupi.
Hadi umauti unamkuta Fred alikuwa ni Mkuu wa Kitengo cha habari cha Tumaini Media, yaani Redio na TV Tumaini.
Marehemu Fred Mosha atakumbukwa kwa mengi ikiwemo uchambuzi wa nyimbo za zamani kutoka Redio Tumaini, kipindi ambacho kilikuwa kinaruka kila siku za Jumamosi kuanzia saa tano asubuhi hadi saa saba mchana.
Ni miongoni mwa waasisi wa vipindi vya michezo mwanzoni mwa miaka ya 2000.
Alikuwa ni mjuzi wa mambo mengi kwani alikuwa na uwezo mkubwa wa kutunza kumbukumbu na kuchambua siasa, muziki na michezo na kupelekea watu kumpa jina la utani la google.
Fred Mosha alikuwa ni mmoja kati ya watangazaji waliobuni na kushiriki staili ya kutangaza soka la Ulaya kwa njia ya TV.
Hiyo ilifanywa kwa mara ya kwanza na Redio Tumaini kwenye fainali za kombe la dunia la mwaka 1998.
Watangazaji wa fainali hizo wakati huo walikuwa ni Fred mwenyewe, Tom Chilala na Victor Robert Wille.
Mchambuzi alikuwa ni kocha Joseph Kanakamfumo.
Baada ya hapo media zingine zikafuata staili hiyo.
Mahali pa msiba na taratibu za maziko bado hazijafahamika kwasababu kauli ya wanandugu bado haijatolewa.
MPANDUKA BLOG itaendelea kukujuza kinachoendelea.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.Amina!

0 comments:
Post a Comment