TAIFA STARS YATUA NAIROBI BILA CANAVARO NA SAMATTA

Kikosi cha timu ya Taifa Stars kimewasili salama nchini Kenya asubuhi ya leo tayari kwa mechi ya kimataifa ya kirafiki itakayofanyika Mei 29 mwaka huu.

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Shirikisho la soka nchini TFF Alfred Lucas, Stars imewasili Kenya mapema leo hii na kufikia katika hoteli ya Safari Club iliyopo jijini Nairobi.

Stars imetua Nairobi bila ya beki Nadir Haroub na Mbwana Samatta.

Nadir ameendelea kushikilia msimamo wake wa kutoichezea timu hiyo huku Samatta akiwa Ubelgiji akikabiliwa na ratiba ngumu na klabu yake ya Genk.

Kikosi cha Stars kina makipa, Deogratius Munishi (Young Africans), Aishi Manula (Azam FC) na Benny Kakolanya (Tanzania Prisons) wakati mabeki ni Mwinyi Haji na Juma Abdul (Young Africans), Aggrey Moris, David Mwantika na Erasto Nyoni (Azam FC), Mohammed Hussein (Simba) na Vicent Andrew (Mtibwa Sugar).

Viungo ni Himid Mao, Farid Mussa (Azam), Jonas Mkude na Mwinyi Kazimoto (Simba), Mohammed Ibrahim na Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar), Ismail Issa (JKT Ruvu), Juma Mahadhi (Coastal Union) na Hassan Kabunda (Mwadui FC) wakati washambuliaji ni Thomas Ulimwengu (TP Mazembe), Mbwana Samatta (KDC Genk), Elias Maguli (Stand United), Ibrahim Ajib (Simba), John Bocco (Azam), Deus Kaseke (Young Africans) na Jeremiah Juma (Tanzania Prisons).
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment