Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusufu Manji mchana wa leo amechukua fomu za kutetea nafasi hiyo katika ichaguzi uliopangwa kufanyika mwezi huu.
Manji hakuchukua fomu hiyo TFF ambako ndiko mchakato huo unaendeshwa na badala yake alichukua fomu katika makao makuu ya klabu ya Yanga ambao leo wameanza rasmi kutoa fomu ikiwa ni utekelezaji wa msimamo wao wa kuendesha uchaguzi wao wenyewe.
Kwa mujibu wa msimamo huo,Yanga imepanga kuwa uchaguzi wao utafanyika Juni 11 mwaka huu, ambayo inapingana na ile ya TFF ya Juni 25.
Manji aliongozana na Clement Sanga ambaye alichukua pia fomu ya kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Yanga.
Kabla ya Manji kuchukua fomu, alizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari na kueleza sababu zilizomsukuma kuchukua fomu kwa ajili ya kutetea nafasi yake kama Mwenyekiti wa klabu hiyo iliyotwaa taji la ligi kuu pamoja na FA msimu huu.
“Nataka kugombea nafasi ya uenyekiti wa Yanga kwa sababu ninauchungu na maendeleo ya klabu hii, nataka ipate mafanikio zaidi ya haya. Yanga ni klabu kubwa lakini bado masikini, viongozi waliopita walikuwa hapa kwa maslahi binafsi kwasababu walisaini mikataba ambayo inaimiza Yanga hadi leo kwa kuikosesha mapato”.
Manji amesema viongozi waliotangulia walisaini mikataba ya haki za televisheni ambayo pesa zake ni ndogo ukilinganisha na mapato ya mlangoni yaliyokuwa yanapatikana kabla ya mechi za ligi ya Vodacom haijaanza kurushwa live kupitia televisheni.
“Pesa iliyokuwa inapatikana zamani wakati mechi hazioneshwi, ni nyingi ukilinganisha na ile ambayo tunaipata kutokana na haki za television. Zamani tulikuwa tunapata karibu milioni 100 hata tukicheza na na Coastal Union, lakini sikuhizi hata watu wa Mbezi hawaji uwanjani kwasababu wanaangalia mpira kwenye TV. Ilitakiwa viongozi waliopo madarakani wajiridhishe kabla ya kusaini mikataba ambayo inaendelea kuikosesha Yanga mapato.”
Baada ya kuzungumza na waandishi wa habari, Manji alianza kazi ya kutumbua majipu ndani ya Yanga kwa kuwasimamisha uanachama baadhi ya viongozi wa klabu hiyo kutokana na viongozi hao kushukiwa kuihujumu klabu.
Manji amemsimamisha uanachama Mwenyekiti wa matawi ya klabu hiyo, Mzee Mohammed Msumi baada ya kugundulika kutaka kuhujumu mchakato wa uchaguzi kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa TFF na BMT.
Katika kuthibitisha hilo, Manji alitoa ushahidi wa sauti ya Msumi akisikika kupanga mikakati ya kukatwa kwa jina la Manji katika uchaguzi ili kumrejesha katibu mkuu wa zamani, Jonas Tiboroha.
“Kwa mamlaka niliyonayo kama Mwenyekiti nimemsimamisha uanachama Msumi kwa kupanga hujuma dhidi yangu katika Uchaguzi huu, na atatakiwa kujieleza kwenye kamati ya nidhamu na maadili” amesema Manji.

0 comments:
Post a Comment