Bale(kulia) |
Mchezaji wa Real Madrid Gareth Bale
amesema kuwa yuko tayari kukabiliana na Barcelona wakati ambapo klabu yake
inajiandaa kupimana nguvu na wapinzani wao Barcelona katika mchezo wa leo wa El
Classico.
Raia huyo wa Wales mwenye umri wa miaka
26,alipata jeraha la nyonga mnamo mwezi Oktoba na alikosa kucheza mechi nne
kabla ya kurudi tarehe 8 Novemba ambapo klabu yake ilishindwa na Sevilla.
''Nimekuwa nje nikiuguza jeraha kwa
wiki sita,kwa hivyo sijapata fursa ya kucheza mechi nyingi msimu
huu'',alisema.lakini sasa najihisi niko tayari kwa mechi hii''.
Bale alikosa kucheza katika mechi ya
kirafiki kati ya Wales na Uholanzi ambapo timu hiyo ilishindwa 3-2.
Real Madrid inacheza mechi hiyo
ikiwa nyuma ya viongozi Barcelona kwa pointi tatu
0 comments:
Post a Comment