Nyota wa Hollywood, Jean-Claude Van Damme ametua katika mazoezi ya Manchester
City na kujumuika na wachezaji mbalimbali wa kikosi hicho.
Van Damme maarufu kama 'Muscles from Brussels' alijumuika na Yaya Toure,
Sergio Aguero na wachezaji wengine ikiwa ni pamoja na kupiga picha pamoja.
Wabelgiji Vincent Kompany na Kevin De Bruyne pia walijumuika na mkali huyo
hiyo jana ambaye alichangamsha sana mazoezi yao kwa kuwa wengi walionekana
kufurahia kumuona.
0 comments:
Post a Comment