Kocha wa zamani wa Aston Villa Paul Lambert
ameteuliwa kocha mpya wa klabu ya Blackburn Rovers baada ya Gary Bowyer kufutwa
kazi.
Lambert mwenye umri wa miaka 46 alifukuzwa na klabu
hiyo ya Aston Villa mwezi Februari ambapo anasema kuwa kwa kipindi kifupi
ambacho amekuwa nje ya timu hiyo anajiona aliyeimarika zaidi na kwamba kwa sasa
anaangalia mbele.
Bowyer alitimuliwa kutokana na kufanya vibaya kwa
klabu biyo. Kati ya mechi 10 za ligi walizocheza alishinda mbili tu na kuifanya
klabu yake ya Rovers kushika nafasi ya 16 katika msimamo wa ligi.
0 comments:
Post a Comment