Timu za Uganda, DR Congo, Morocco, Guinea na Gabon
zimesonga mbele katika hatua ya makundi ya kusaka tiketi ya Kombe la Dunia.
Uganda, wakicheza nyumbani katika uwanja wa Mandela
waliifunga Togo 3-0 na hivyo wakawa wameshinda kwa jumla ya mabao 4-0 ambapo
mchezo wa kwanza walishinda kwa bao 1-0.
Gabon nao wakasonga mbele katika hatua ya makundi
kwa ushindi wa mikwaju ya penalti 4-3 dhidi ya Msumbiji.
Nao Zambia, wakawachapa Sudan kwa 2-0 na kufuzu kwa
makundi kwa jumla ya mabao 3-0 huku mabao ya jana yakifungwa na Lubambo Musonda
na Winston Kalengo.
DR Congo walitoka sare ya 2-2 na Burundi huko kwao
lakini wamesonga mbele baada ya kushinda mchezo wa kwanza kwa mabao 3-2 huko
Bujumbura.
Morocco nao wamefuzu licha ya kufungwa 1-0 jana na
Equatorial Guinea baada ya wao kushinda mechi ya kwanza 2-0.
Timu hizi 6 zilizofuzu zitaungana na nchi nyingine
14 zitakazofuzu Jumanne na kupangiwa makundi matano ya timu 4 kila kundi.
Mshindi mmoja wa kila kundi atafuzu kwa fainali za
Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Urusi.
0 comments:
Post a Comment