MAN UNITED YAMFUKUZIA CRISTIANO RONALDO

Kocha mkuu wa Manchester United Louis van Gaal amesema akifanikiwa kumsajili nyota Cristiano Ronaldo litakuwa jambo jema zaidi.

Kumekuwepo na taarifa siku za hivi karibuni kwamba Ronaldo ambaye jana alicheza kwenye mechi ya kipigo cha 4-0 vs Barcelona – kwamba ataondoka Madrid mwishoni mwa msimu huu.

Van Gaal hivi karibuni alizungumzia kuhusu usajili anaotaka kuufanya katika kuimarisha kikosi chake na Mdachi huyo ameonekana kuwa na matumaini ya kufanya kazi na Ronaldo.

“Anacheza upande wa winga na ana kasi sana, pia anafunga magoli. Sidhani kama kuna kocha duniani ambaye hapendi kuwa naye kikosini,” Van Gaal amekaririwa kwenye magazeti ya leo ya UK.

“Ni kweli tunajaribu kusajili wachezaji wazuri wakubwa na sio Ronaldo pekee yake, lakini sio rahisi kuwapata aina hii ya wachezaji.

“Tusubiri tukiendelea kutumaini.”

Ronaldo, 30, ana mkataba na Madrid mpaka 2018, japokuwa kwa sasa hali inazidi kuonyesha wazi mshambuliaji huyo ataihama Madrid mwishoni mwa msimu huu. 
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment