MASHABIKI WAMKOMALIA PEREZ,WAMTAKA AJIUZULU

Mashabiki wa klabu ya soka ya Real Madrid wamekuja juu na kumshinikiza rais wao Florentino Perez aachie ngazi.

Real Madrid pamoja na kuwa nyumbani, imekumbana na kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa wapinzani wake hao wakubwa Barcelona.

Hasira za mashabiki wa Real Madrid sasa zimemuangukia Rais wa klabu hiyo, Florentino Perez na wanataka ajiuzulu.


Uamuzi huo unatokana na wao kuamini hawajibiki ipasavyo na timu hiyo imeingia katika matatizo makubwa ya kushindwa kucheza kwa kiwango huku yeye akiwa kimya.


Mashabiki hao wanaona wamepata aibu kubwa, kwani licha ya kuchapwa mabao hayo manne, lakini Barcelona ndiyo waliotawala mchezo wa dakika zote 90 hiyo jana huku wakionyesha soka la kuvutia.

Mashabiki waliokuwa uwanjani, walikuwa wakizomea huku wakiangalia upande aliokaa Perez ambaye walimuonyesha wanataka aachie ngazi.

Mashabiki waliokuwa uwanjani, walikuwa wakizomea huku wakiangalia upande aliokaa Perez ambaye walimuonyesha wanataka aachie ngazi.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment