Waziri wa michezo wa Ufaransa, Thierry Braillard
amebainisha kuwa mechi za Ligi Kuu ya nchi hiyo maarufu kama Ligue 1 na ligi
daraja pili au Ligue 2 zinatarajiwa kuendelea kama zilizopangwa mwishoni mwa
wiki hii, wiki moja baada ya mashabulio ya kigaidi jijini Paris.
Mwishoni mwa wiki iliyopita ratiba kadhaa za michezo
ndani na maeneo mengine kuzunguko mji huo zilisimamishwa kufuatia matukio hayo
ya kigaidi ambayo yamepeleka vifo vya zaidi ya watu 129.
Kufuatia kikao cha kati ya wizara ya mambo ya ndani
na Bodi ya Ligi ya nchi hiyo, Braillard amesema waliafikiana kuwa mechi za ligi
za mwishoni mwa wiki hii ziendelee kuchezwa kama zilivyopangwa.
Kikubwa kitakachofanyika katika mechi hizo ni
kuongeza hali ya usalama katika maeneo yote ya nchi hiyo ili kuhakikisha hakuna
tukio lingine linatokea.
0 comments:
Post a Comment