Na Nicolaus Kilowoko
Uongozi wa klabu ya soka ya Simba
umeitaka klabu ya soka ya Etoile Du Sahel ya nchini Tunisia kuhakikisha
inawalipa mapema fedha za aliyekuwa mchezaji wao Emmanuel Okwi kabla ya kufikia mwezi Machi mwakani.
Akizungumza na waandishi wa habari
msemaji wa klabu hiyo Haji Manara amesema klabu hiyo ya Etoile Du Sahel
iliandika barua kwenda Shirikisho la soka la Dunia FIFA kutaka kuongezewa muda
wa kulipa deni lao ndani ya klabu ya Simba hadi mwezi Machi mwakani, jambo
ambalo uongozi wa Simba umepinga suala hilo.
Klabu ya Simba inaidai klabu ya
Etoile Du Sahel takrimbani sh. milioni 600 kwa ajili ya mchezaji wao Emmanuel
Okwi ambazo hazijalipwa hadi sasa ndani ya klabu hiyo.
“Imekuwa ni tabia yao kutuzungusha,
kila unapokaribia muda wa kulipa deni huandika barua FIFA na kuomba waongezewe
muda.Tumeshachoshwa na hali hii”
Okwi alinunuliwa na Etoile Januari
mwaka 2013 kwa dau la dola 300,000 ambazo ni sawa na shilingi milioni 600 za
kitanzania ingawa baada ya muda akaingia kwenye mgogoro na klabu hiyo ya
Tunisia.
Mtafaruku ulianza baada ya Okwi
kuchelewa kurejea mjini Sousse mkoani Sahel baada ya ruhusa ya kwenda kuichezea
timu yake ya taifa, Uganda.
Okwi naye akadai Etoile walikuwa
hawamlipi mishahara na kufungua kesi FIFA (Shirikisho la Soka la Kimataifa),
ambayo mwisho wa siku alishinda kwa kuruhusiwa kutafuta timu nyingine ya
kuchezea kulinda kipaji chake, wakati akisubiri suluhisho la mgogoro wake na
klabu ya Tunisia.
Hata hivyo, Okwi mwaka huu Simba ilimuuza katika klabu ya
Sonderjyske FC inayoshiriki ya Ligi Kuu ya Denmark ambako amesaini mkataba wa
miaka mitano.
0 comments:
Post a Comment