Kocha mkuu wa Bayern Munich, Pep Guardiola amewasili
nchini Kenya kwa safari binafsi ya mapumziko ya mwishoni mwa mwaka ikiwa ni
pamoja na kufanya utalii.
Guardiola alitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa
wa Jomo Kenyata (JKIA) akiwa ameongozana na mkewe Cristina Serra, na watoto wao
Maria Guardiola, Marius Guardiola na Valentina Guardiola.
Baada ya kuwasili, kocha huyo anayeheshimika sana
barani Ulaya alijipiga picha marufu kama 'selfie' na mashabiki wake raia wa
Kenya ikiwa ni pamoja na Gavana wa Mombasa, Ali Hassan Joho.
Akizungumza na waandishi wa habari, Joho amesema
Guardiola amefurahi kufika nchini Kenya na atakuwepo hadi mwaka mpya.
"Amefurahi sana kufika Kenya, atakuwepo hadi
baada ya mwaka mpya ila amesema atahitaji utulivu kwa ajili kupumzika na
familia yake,"alisema Joho.
Gavana Joho amemwalika kocha huyo anayeondoka Bayern
kutembelea fukwe maridhawa za Mombasa.
0 comments:
Post a Comment