ARSENAL KWA CHELSEA BADO LAINIII!

Arsenal leo imekubali uteja wa kudumu kwa Chelsew baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England uliopigwa usiku huu.

Arsenal imejikuta ikifa nyumbani Emirates kwa bao la dakika ya 23 la mtukutu Diego Costa aliyeunganisha mpira wa krosi.

Katika mchezo huo Chelsea ilionekana kucheza kwa kujiamini zaidi na kutawala mchezo kufuatia mmoja kati ya wachezaji wa Arsenal kulambwa kadi nyekundu mapema kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili Arsenal ilimuingiza Alexis Sanchez ambaye kwa kiasi fulani alionesha uhai ingawa umaliziaji ulikuwa butu.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment