MSUVA AITAKATISHA YANGA FA CUP

Yanga imeituliza Friends Rangers kwa mabao 3-0 katika mechi ya Kombe la FA linalodhaminiwa na Azam Sports.

Mechi hiyo imepigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na mabao ya Yanga yakifungwa na Simon Msuva (mawili) na Matheo Simon aliyemalizia la tatu.

Simba jana ilishinda kwa mabao 3-0 dhidi ya Burkina Faso ya Morogoro katika mechi nyingine ya Kombe la Shirikisho.
Kocha Hans van der Pluijm alipanga wachezaji kadhaa ambao wamekuwa hawapati nafasi.

Friends Rangers wanaonolewa na Ally Yusuf Tigana, walionekana kucharuka mara kadhaa na kufanya mashambulizi lakini hawakuwa na shabaha.


Hata hivyo, mabeki wa Friends, mara kadhaa walionekana kama waliopigwa ganzi kutokana na kutochangamka na kusababisha mabao mawili ambayo yalionekana kuwa ni 
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment