Hatma ya kocha wa Manchester United Louis van Gaal
imeonekana kuwa shakani baada ya kocha huyo kusitisha ghafla program ya mazoezi
na kutimkia nchini Uholanzi.
Taarifa zinaeleza kwamba Jumapili kocha huyo
alisitisha mazoezi na kukimbilia nchini Uholanzi huku jukumu akimkabidhi
mkongwe Ryan Giggs.
Van Gaal alifanya uamuzi huo ikiwa ni siku moja
baada ya United kufungwa bao 1-0 na Southampton katika mchezo wa Ligi Kuu.
Van Gaal aliwaambia wachezaji wake wasiende kwenye
viwanja vya mazoezi vya Carrington.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 64 aliaga kwmaba
anakwenda Uholanzi kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mtoto wake wa kike.
Lakini hali hiyo imehusishwa na mustakabali wake
ndani ya timu hiyo kwamba huenda asidumu sana Old Trafford.
0 comments:
Post a Comment