Timu mbili zitakazofuzu nusu fainali kutoka kundi “B” kwenye Kombe la mapinduzi zitajulikana leo hii baada ya michezo miwili kumalizika.
Saa 10:15 za jioni wataanza Azam na Mafunzo, na saa 2:15 usiku watamalizana kati ya Yanga na Mtibwa Sugar michezo yote itasukumwa kwenye uwanja wa Amaan.
Mchezo wa awali kati ya Azam na Mafunzo , Mafunzo hata akishinda hatakwenda nusu fainali kwani ameshaaga rasmi leo anakamilisha ratiba tu kufuatia michezo yake miwili ya awali kufungwa na Yanga 3-0, na wa pili kufungwa na Mtibwa Sugar 1-0.
Azam analazimika ashinde kwenye mchezo huo ndipo atakata tiketi ya kucheza nusu fainali, lakini akipoteza au akienda sare atawasaidia Yanga na Mtibwa kufuzu nusu fainali kiulaini.
Sare kwa Yanga itawasaidia kutinga nusu fainali, lakini akifungwa Yanga ataaga rasmi kwenye kombe hilo, ndipo hapo mchezo huu unazidi kuwa mgumu sana kutokana na mazingira halisi yaliyopo.

0 comments:
Post a Comment