MAREFA WALIOBORONGA MECHI YA YANGA NA AZAM KUKIONA

Chama cha soka cha Zanzibar ZFA kimekiri kwamba waamuzi waliochezesha mchezo wa juzi kati ya Yanga na Azam waliboronga.

Akizungumza na MPANDUKA BLOG, Mkurugenzi wa ufundi wa ZFA Masoud Attai alisema wanachokifanya kwa sasa ni kutazama kwa umakini video za mechi hiyo na kisha itachukua hatua stahiki.

Alisema waamuzi wameonyesha udhaifu katika mashindano haya hasa kulingana na msukumo wa upinzani kwa timu zinazochuana.

"Tumeshamsimamisha mmoja ambaye alichezesha mechi ya Mtibwa na Azam na kuwapa onyo waamuzi wawili na sasa huenda tukatoa adhabu kali kwa waliochezesha mechi ya Yanga na Azam pindi tutakapojiridhisha kwamba ni kwa kiwango gani mechi iliwaelemea" alisema Attai.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment