Kocha mkuu wa Arsenal, Arsene Wenger amelalamika vikali
dhidi ya hujuma na hila za mshambuliaji machachari wa Chelsea Diego Costa
aliyesababisha mchezaji wake Per Mertesacker kutolewa mapema katika mechi
iliyochezwa kwenye dimba la Emirates.
Katika mechi hiyo ya Ligi kuu ya Uingereza Chelsea
ilibuka na ushindi wa bao 1-0.
Mfungaji wa bao hilo alikuwa ni mshambuliaji huyo
mtukutu Diego Costa.
Mjerumani Per Mertesacker aliamrishwa kuingia bafuni
mapema baada ya kuoneshwa kadi nyekundu kunako dakika ya 18 ya kipindi cha kwanza
kwa kumuangusha Costa.
Kufuatia kuondoka kwa Mertesacker mapema sana katika
mechi hiyo, Arsenal ilipoteza kasi mbali na uongozi wake kileleni mwa ligi kuu.
Hivyo kocha Arsene Wenger amesema mwamuzi
Clattenberg aliwaonea kwa kutoa kadi hiyo na kwamba hata Costa alileta hila na
kufanya beki huyo apewe kadi.
Arsenal sasa wameshuka hadi nafasi ya 3 wakiwa na
jumla ya pointi 44.
Manchester City ambao walisajili ushindi muhimu
wamewapiku Arsenal kutoka nafasi ya pili kwa wingi wa mabao.
0 comments:
Post a Comment