Timu ya soka ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ Mei 19, 2016 imetinga hatua ya Nusu Fainali baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 na Korea Kusini katika mfululizo wa michuano maalumu ya kimataifa yaliyoandaliwa na Shirikisho la Soka nchini humo (AIF Youth Cup 2016 U-16).
Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Tilak, Maidan mjini Goa, India mabao ya Serengeti yalifungwa na Assad Juma katika dakika ya 12 na Maulid Lembe katika dakika ya 87 ambaye alisawazisha baada ya Korea kutangulia kwa mabao 2-1.
Matokeo hayo yanaifanya Serengeti Boys ifikishe pointi tano na kwamba inasubiri matokeo ya mwisho kati ya Korea Kusini na Marekani yatakayotoa mwanga wa timu itakayocheza fainali.

0 comments:
Post a Comment