MCHEZO wa kukunja sura ni mchezo ambao watu
hushindana kukunja sura zao kwa mitindo tofauti tofauti.
Mchezo huo huusisha viungo mbalimbali vilivyopo
katika sura ya mtu kama vile macho, pua, midomo, kidevu na hata mashavu.
Hivyo washindani hutumia viungo hivyo kwa ajili ya
kutafuta ushindi dhidi ya wengine.
Wapo washindani wanawaotumia kiungo kimoja cha sura
yao na pia wapo wanaotumia viungo vyote ilimradi kufanya sura itishe kuliko mtu
mwingine na kuweza kujinyakulia ushindi.
Mbali na hilo, wapo watu wanaodiriki hata kulia ili
sura iweze kujikunja yenyewe na kutoa muonekano wa kutisha zaidi ya wengine kwa
lengo la kujinyakulia ushindi.
Mchezo huu hufanyika sana katika nchi za Ulaya
ambazo hadi sasa zinashikilia rekodi ya kuwa na michezo mingi zaidi kuliko zile
za Barani Afrika.
Bado haijafahamika kwamba mchezo huu asili yake ni
nchi gani na badala yake umeonekana ukishindaniwa katika nchi mbalimbali za
Ulaya.
Mashindano hayo yalianza katika miaka ya zamani ambapo
kuanzia mwaka 1267, mchezo ulikuwa unachezwa kwa mwaka mara moja kule nchini
Uingereza.
Mnamo mwaka 1852 gazeti la Cumberland Paquet
liliwahi kuuelezea mchezo huo kama mchezo wa kitamaduni.
ULIANZIA
VIJIJINI
Katika miaka hiyo mashindano yalikuwa yanafanyika
kiholela katika vijiji mbalimbali ambapo washindani walikuwa wakishindana kwa
kukunja sura zao kwa mitindo tofauti.
Mashindano ya dunia ya kukunja sura yalikuwa
yanafanyika kila mwaka mara moja katika eneo la Egremont, Cumbria.
Kwa washindani ambao walikua na vinywa vilivyokosa
meno, walikua na nafasi kubwa zaidi ya kupata ushindi kwa sababu walikuwa na
uwezo wa kuacha wazi vinywa vyao na kuchagiza kutisha kwa sura.
Peter Jackman alikuwa kinara wa sura ya kutisha
baada ya kutwaa taji la dunia mara nne, akianzia mwaka 1998 na kupachikwa jina
la ‘Bela Lugosi’
Pia alifanya kazi nyingi na Televisheni ikiwemo
muonekano wake katika kipindi cha BBC kilichojulikana kama ‘They Think It's All
Over’.
Mnamo mwaka 2000 alilazimika kuondoa meno yake ili
kuwa na muonekano tofauti.
Mwanamke pekee kuweka rekodi kubwa katika mashindano
ya dunia ni yule aliyeshinda taji mara 15, Tommy Mattinson kutoka UK.
Alifanya hivyo kati ya mwaka 1986-87 na kisha mara
10 kati ya mwaka 1999 na 2010.
JINSI
MCHEZO UNAVYOSHINDANIWA
Mchezo huu unaonekana kama wa kitoto hivi hasa pale
watu wazima wanapoamua kushindana kukunja sura zao.
Mashindano hayo hushindaniwa kwa namna mbili tofauti
ikiwemo ya kukusanya picha za washindi mbalimbali waliokunja sura zao.
Namna nyingine ni kuwashindanisha watu ana kwa ana
ambapo mshindani anakuwa anaonyesha mbwembwe zake.
Ushindi huwa unatolewa hasa kwa yule ambaye sura
yake imeonekana kutisha zaidi ya mwingine.
Kwa mshindani ambaye atashindwa kutumia vema viungo
vyake vya sura, huwa na uwezekano mkubwa wa kupoteza ushindi.
Athari kuu ya mchezo huu kwa mwanamichezo
anayeshindana mara kwa mara ni kuifanya sura yake izeeke haraka hata kama umri
bado ni wa ujana.
Makala
imeandaliwa na Arone Mpanduka kwa msaada wa mtandao wa intaneti. Barua pepe- mpanduka@yahoo.com
0 comments:
Post a Comment