TRAFIKI MDAU WA YANGA AFARIKI DUNIA

Askari wa usalama barabarani ambaye pia ni mdau mkubwa wa michezo na klabu ya Yanga Sajenti Ally Kinyogori amepigwa risasi jana usiku akiwa nyumbani kwake.

Taarifa zinadai kwamba, mnamo tarehe May 19, 2016 Sgt Kinyogori baada ya kutimiza majukumu yake ya kikazi traffic makao makuu alirejea nyumbani kwake huko Mwandege, Mkuranga mpakani mwa Dar es Salaam na Pwani.

Akiwa sebuleni kwake majira ya saa 3 usiku, watu wasiojulikana waliingia ndani na kumpiga risasi moja kifuani na nyingine ubavuni kisha kutoweka bila kuchukua kitu chochote. Alikimbizwa hospitali akiwa hajitambui na baadaye kufariki dunia.

Kinyogori alikuwa karibu na viongozi na wadau mbalimbali wa michezo na alikuwa akitoa msaada mkubwa pale timu zinapokwama kwenye foleni kwa kuwasiliana na askari waliokaribu na eneo husika pindi anapopokea taarifa kutoka kwa viongozi wa timu.

Kinyogori mara kwa mara alikuwa akisikika asubuhi kupitia kituo cha Radio One katika kipindi cha Kumepambazuka akitoa taarifa mbalimbali za barabarani za eneo lake la kazi.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment