TIMU ZA TANGA ZASHUKA.DARAJA, SIMBA SC 'YAIOKOA'RUVU JKT

Timu za soka za Mgambo JKT na African Sports leo zimeungana na Coastal Union (zote kutoka Tanga )kushuka daraja baada ya kuboronga katika msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Hiyo inamaanisha kwamba jiji la Tanga msimu ujao halitakuwa na muwakilishi yoyote katika Ligi Kuu.

Msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara wa 2015/16 umefikia tamati leo kwa mechi zote kuchezwa huku Yanga ikiwa tayari imetwaa ubingwa wake.

Ligi hiyo ilianza Septemba 12 mwaka jana na kuhitimishwa leo.

Burudani nyingine ya soka nchini Tanzania itakuwepo Jumatano ijayo ambapo Yanga itavaana na Azam FC katika mchezo wa fainali ya kombe la FA.

MATOKEO YA LEO YA VPL

Azam 1, Mgambo 1
Majimaji 2, Yanga 2
Simba 1, JKT 2
Toto 0, Stand 1
Mwadui 0, Kagera 2
Mtibwa 2, African Sport 0
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment