MAN UNITED KUMTANGAZA MOURINHO LEO

Manchester United wanategemea kumtangaza Jose Mourinho kuwa kocha wao mkuu leo, tangazo rasmi la usajili wa kocha huyo linategemewa kutolewa leo baada ya mchezo wa fainali ya FA Cup baina ya Manchester United vs Crystal Palace.

Majadiliano ya mkataba wa miaka 3 yalifanyika baina ya CEO wa United Ed Woodward na wakala wa Mourinho, Jorge Mendes wiki kadhaa zilizopita; japokuwa kumekuwepo na sintofahamu kubwa juu ya usajili wa Mourinho kwenye bodi ya wakurugenzi wa Man United. Lakini baada ya majadiliano marefu maamuzi yakafikiwa kwamba haijalishi na matokeo yatakayotokea leo pale Wembley, utawala wa Van Gaal umefikia tamati.

Mourinho alisaini makubaliano ya kabla ya mkataba wa kazi rasmi, ambao uliweka wazi kama kocha huyo hatopewa timu mwishoni mwa msimu basi angelipwa mamilioni ya fedha na Man United. 
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment