LONDON,England
Chelsea ya England inashuka
uwanjani usiku wa leo kucheza mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Dynamo
Kiev.
Pamoja na kutofanya vema, wachezaji wa Chelsea wameonekana
kuwa na furaha kabisa tayari kwa mchezo huo wa leo.
Kocha Mkuu, Jose Mourinho
na watu wake wa benchi la ufundi nao wameonekana kuwa na furaha utafikiri
hakuna tatizo.
Chelsea imekuwa ikiyumba
katika mechi za Ligi Kuu England pamoja na michuano mingine yote hali ambayo
imeanzisha hofu kwa Mourinho atatimuliwa.
Huenda mechi hiyo ya
Ligi ya Mabingwa Ulaya, leo na ile ya Ligi Kuu England dhidi ya Stoke City,
Jumamosi itakuwa ni sehemu ya mwisho wa uamuzi wa klabu ya Chelsea kubaki au
kuachana na Mourinho.
0 comments:
Post a Comment