JANUARI
Simba yatwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi baada ya
kuifunga Mtibwa Sugar penati 4-3 baada ya suluhu ya 0-0 katika dakika 120.
Shujaa wa mchezo alikuwa kipa wa Simba kwa wakati
huo Ivo Mapunda baada ya kupangua moja ya penati hizo.(Hiyo ilikuwa ni usiku wa Januari 13, siku ya Jumanne kwenye dimba la
Aman)
FEBRUARI
Februari 2 bondia Francis Cheka alihukumiwa kwenda
jela kutumikia kifungo cha miaka mitatu.
Hukumu hiyo ilitolewa Morogoro baada ya bodnia huyo
kubainika kwa kosa la kumpiga mfanyakazi wa Bar huko Morogoro, tukio ambalo
lilitokea mwaka 2014.
February 6 mchezaji wa Mbeya City Juma Nyosso
alifungiwa mechi 8 kwa kosa la kumdhalilisha aliyekuwa mchezaji wa Simba Elias
Maguli.
Nyosso alifanya hivyo kwenye mchezo kati ya Mbeya
City na Simba.
MACHI
Machi 25 mwaka huu mwanachama wa ‘Simba Ukawa’
Hassan Msumari nusura apate kichapo baada ya kwenda katika jengo la Yanga kwa
lengo la kuzungumza na waandishi wa nabari waliokwenda huko kwa lengo la
kufanya mkunano na uongozi wa Yanga.
Msumari ambaye mwenyekiti wa Chama cha Muziki wa
Dansi nchini alikwenda Yanga kwa lengo la kukutana na waandishi ili awape
habari zinazohusu chama hicho lakini katika hali ya kushangaza Yanga walidai
kwamba Msumari alitumwa na klabu ya Simba ili kwenda kufanya ushirikina klabuni
hapo.
Hata hivyo gari la polisi ilikuja na kumuokoa ili
aipewe kichapo na wanachama wa Yanga waliokuwepo klabuni hapo wakiongozwa na
mzee Akilimali.
Machi 27 bondia Mohamed Matumla alishinda pambano la
masumbwi la raundi 10 kwa kumchakaza Mchina Wang Xiu Hua.Pambano lilifanyika
ukumbi wa Diamond Jubilee.
APRILI
Aprili 27 Yanga ilijitangazia ubingwa wa Ligi Kuu
mapema baada ya kuinyuka Polisi Moro mabao 4-1 kwenye mechi iliyopigwa uwanja
wa Taifa jijini Dar es salaam.
Yanga ilitawazwa bingwa baada ya mechi hiyo licha ya
kuwa ilibakisha mechi kadhaa za kumaliza Ligi.
MEI
Mei
8 mwaka huu TFF ilimpiga faini ya shilingi milioni 5
msemaji wa Yanga Jerry Murro kwa kosa la kumrushia maneno yasiyofaa aliyekuwa
kaimu mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi.
Kisa kilikuwa ni kupinga kanuni ya ajabu ya mchezaji
mwenye kadi mbli za njano kuruhusiwa kuchagua mchezo wa kutumikia adhabu.
Mwishoni
mwa mwezi Mei mwaka huu, aliyekuwa kiungo wa Simba Ramadhan
Singano aliibua mjadala mzito kwenye vyombo vya habari baada ya kulalamika
kwamba Uongozi wa Simba ulighushi mkataba wake.
Singano alidai kwamba mkataba wake ni wa miaka miwli
na ulikuwa uishe mwaka huu lakini Simba ilidai Messi kasaini mkataba wa miaka
mitatu hivyo hakuna haja ya kumuongezea mkataba mpya ilhali alikuwa na mwaka
mmoja mbele.
JUNI
Katika hali ya kushangaza Juni 9 mwaka huu, TFF
ilitoa maamuzi ya kutatanisha juu ya sakata la Singano na Simba. Katibu mkuu wa
TFF Celestine Mwesigwa alisema wamezitaka pande zote mbili kukaa na kukubaliana
kumsainisha mkataba mpya mchezaji huyo
Hata hivyo Singano alionekana kutoridhishwa na
maamuzi hayo na kusema kwamba anamuachia Mungu
Juni
23
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania – TFF, Jamal Malinzi alizungumza
na waandishi wa habari katika ukumbi wa hoteli ya Tansoma eneo la Gerezani na
kumtangaza Charles Mkwasa kuwa kocha mkuu wa muda baada ya Mart Nooij
kutimuliwa.
Mkwasa alipewa mkataba wa muda wa miezi 3 hadi
Septemba 30 na kisha kupewa wa kudumu.
JULAI
Julai 9 mwaka huu Rais mstaafu wa awamu ya nne
Jakaya Kikwete alisema watu wanamfikiria vibaya kwamba akienda kutazama mechi
za Timu ya Taifa Stars huwa hazifanyi vizuri.
Maneno hayo aliyasema wakati akivunja rasmi Bunge la
10 mjini Dodoma ili kupisha mchakato wa uchaguzi mkuu wa Rais Wabunge na
Madiwani
Julai 23 mwaka huu Yanga ilianza rasmi hadithi za
uchaguzi baada ya muda wa viongozi wa kuchaguliwa kumalizika rasmi.
AGOSTI
Agosti
2
Azam FC ilitwaa kombe la Kagame kwa mara ya kwanza kabisa tangu ianzishwe mwaka
2007 baada ya kuinyuka Gor Mahia mabao 2-0 katika mchezo wa fainali.
Agosti
17
mwaka huu Baraza la Sanaa la Taifa BASATA lilitangaza rasmi kulitoa kifungoni
shindano la Miss Tanzania.
Shindano hilo lilipigwa stop Disemba 22 mwaka jana kufuatia
skendo la kughushi umri ililomkumba Sitti Mtemvu mwishoni mwa mwaka jana na
kulazimika kuvua taji na kumkabidhi Lilian Kamazima
SEPTEMBA
Jumamosi
ya Sept 26 Mchezaji chipukizi wa timu ya vijana ya
Coastal Union ya Tanga, Mshauri Salim alifariki dunia baada ya kuanguka kwenye Uwanja
wa Mkwakwani kufuatia kugongana na mchezaji mwenzake.
Tukio hilo lilitokea katika mchezo wa timu ya vijana
chini ya umri wa miaka 20 ya Coastal Union dhidi ya Eagles Academy uliotangulia
kabla ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Coastal na Mwadui
FC ya Shinyanga uliomalizika kwa sare ya 0-0.
Septemba
30
mwaka huu mchezaji wa Mbeya City Juma Nyosso alipata adhabu nyingine tena kwa
kosa lilelile la udhalilishaji ambapo safari hii alimdhalilisha mchezaji wa
Azam FC John Bocco.
Nyosso alifungiwa kutojihusisha na soka kwa kipindi
cha miaka miwili baada ya kumdhalilisha Bocco kwenye mchezo wa Ligi kuu kati ya
Mbeya City na Azam uliopigwa Jumapili ya Sept 27.
OKTOBA
Oktoba 2 Bondia Cosmas
Cheka, alifanikiwa kuingia kwenye rekodi ya mabondia wa Tanzania waliobeba
ubingwa wa dunia.
Cheka ambaye ni mdogo
wa bingwa mwingine wa dunia, Francis Cheka alimtwanga bondia wa Thailand huko
nchini Thailand na kubeba ubingwa huo wa dunia.
Licha ya kwenye rekodi ya mabondia waliowahi
kubeba ubingwa wa dunia akiwemo kaka yake Cheka, pia ameingia kwenye rekodi ya
mmoja wa mabondia waliobeba ubingwa wa dunia wakiwa nje ya ardhi ya Tanzania.
Wengine waliowahi kubeba ubingwa wa dunia
wakiwa nje ya ardhi ya Tanzania ni marehemu Magoma Shabani aliyebeba ubingwa wa
dunia wa WBU nchini Italia.
NOV
Novemba
17
mwaka huu(Jumanne) aibu ya mwaka iliikumba Taifa Stars kwa kunyukwa mabao 7-0
na Algeria katika mchezo wa kuania kupangwa kwenye makundi ya kufuzu kwa
fainali za kombe la dunia za mwaka 2018.
Mchezo huo ambao ulipigwa nchini Algeria uliifanya
Stars iondoshwe kwenye kinyang’anyiro hicho baada ya mchezo wa awali timu zote
kutoka sare ya 2-2.
Novemba
19
mwaka huu kocha Kassim
Majaliwa ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa alitangazwa rasmi kuwa Waziri mkuu
mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Majaliwa alipata nafasi hiyo baada
ya kuthibitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa wingi wa kura
za ndiyo baada ya jina lake kuwasilishwa Dodoma na Rais John Pombe Magufuli.
Majaliwa ni mmoja kati ya watu
wanaopenda michezo, jambo ambalo lilimfanya asomee ukocha na kupata Leseni B ya
Shirikisho la soka Barani Afrika CAF.
Kufuatia kuwa na taaluma hiyo, Majaliwa
ana uwezo wa kufundisha timu yoyote ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
DEC
Disemba
13
Timu ya taifa ya kuogelea ilitwaa medali 45 kwenye michuano ya Afrika
iliyofanyika Disemba 13 hadi 16 nchini Uganda.
Timu hiyo ilishinda medali 12 za dhahabu, 22 za fdha
na n11 za shaba.
Disemba
28
Yanga ilifanya maamuzi magumu kwa kumtimua Haruna Niyonzima baada ya kuona
kwamba mchezaji huyo amekiuka masharti ya mkataba.
KIMATAIFA
Mchezaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski
alifunga mabao matano ndani ya dakika 9 dhidi ya Wolfsburg(Sept 22)
Sepp Blatter na Michel Platini walipigwa mvua ya
kifungo cha miaka 8 na kamati ya maadili ya FIFA bada ya kubainika kuwa
walifanya ubadhilifu.
Watanzania Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu
walibeba kombe la klabu bingwa Afrika.
Timu ya soka ya taifa ya wanawake ya USA ilichukua
kombe la dunia kwa mara ya tatu na kuwa timu iliyochukua kombe hilo mara
nyingi.
Barcelona imecukua jumla ya makombe matano kwa mwaka
huu.
Leicester City kukaa kileleni mwa EPL sikukuu ya
Krismasi
Cristiano Ronaldo alivunja rekodi ya ufungaji wa
muda wote ndani ya Real Madrid ambayo ilikuwa ikishikiliwa na Raul Gonzalez
mwenye magoli 323.
Chelsea yatwaa taji la Ligi kuu England.Iliifunga
Crystal Palace bao 1-0.
Pambano la masumbwi la bondia Floyd Mayweather na
Manny Paquiao ambapo Mayweather alishinda.
Chelsea yamtimua Jose Mourinho
Uholanzi yashindwa kuuzu michuano ya Euro 2016.
MATUKIO
HAYA YAMETAYARISHWA NA ARONE MPANDUKA
0 comments:
Post a Comment