Rais wa TFF Jamal Malinzi |
Michuano ya Kombe la Shirikisho ya
Azam Sports inafunguliwa rasmi Jumapili (Novemba 8, 2015) kwa mechi tatu
zitakazochezwa kwenye viwanja vitatu tofauti.
Mechi rasmi ya ufunguzi itakuwa kati
ya wenyeji JKT Rwamkoma ya Mara na Villa Squad ya Dar es Salaam
itakayofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.
Siku hiyo pia kutakuwa na mechi kati
ya Kariakoo ya Lindi na Changanyikeni FC ya Dar es Salaam itakayochezwa kwenye
Uwanja wa Ilulu mjini Lindi, wakati Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini
Mbeya utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Wenda FC ya Mbeya na Madini SC ya
Arusha.
Bingwa wa michuano hiyo
inayodhaminiwa na Azam Sports HD ataiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya
Kombe la Shirikisho barani Afrika mwaka 2017.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA
MIGUU TANZANIA (TFF)
0 comments:
Post a Comment