MVUA YATIBUA MECHI YA ARGENTINA NA BRAZIL















Mvua kubwa iliyonyesha katika jiji la Beunos Aires nchini Argentina jana imesababishwa kuahirishwa kwa mchezo wa mzunguko wa tatu wa kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia mwaka 2018 kwa mataifa ya Amerika Kusini kati ya mchezo wa Argentina na Brazil.

Mchezo huo uliahirishwa saa moja kabla ya kuanza kutokana na hali ya uwanja wa Monumental kutokua vizuri huku mashabiki pia wakiwa wamejificha kuogopa kuingia barabarani kutokana na dhahama hiyo.

Akiongea katika taarifa yake kocha msaidizi wa Brazil alisema, “hatukuhofia pitch pekee kwamba tusingecheza mchezo mzuri, bali pia mfumo wa umeme uwanjani ungeweza kuwa hatari zaidi kwetu na mashabiki”.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa leo saa sita usiku (GMT) katika uwanja huo huo wa Monumental huku Argentina ikitarajiwa kuwakosa nyota wake hatari Lionel Messi na Sergio Kun Aguero ambao ni wagonjwa.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment