SAFARI YA SAMATTA ULAYA YAANZA KUPIGWA DANADANA

Safari ya Mbwana Samatta ya kwenda kucheza soka la kulipwa katika nchi za Ulaya imeanza kupigwa danadana.

Samatta ambaye awali ilisemekana kuwa huenda akaenda nchini Ufaransa kucheza soka la kulipwa kabla ya mpango huo kubadilika na kuhamia nchini Ubelgiji kwenye klabu ya Genk, sasa inaelezwa kuwa huenda asijiunge na klabu hiyo.

Meneja wa mchezaji huyo, Jamal Kisongo alisema kuna mpango Samatta akaenda katika klabu ya Standard Liege ya Ubelgiji badala ya Genk kama ilivyoelezwa awali.

Alisema kunachoonekana ni kwamba bado hakuna muafaka kupitia mazungumzo kati ya mmiliki wa TP Mazembe Moise Katumbi na klabu ya Genk.

Alisema bado mjadala mzito unaendelea baina yao na jibu kamili na la uhakika juu ya wapi Samatta atakwenda, litapatikana ndani ya siku hizi mbili.

Kwa sasa Samatta yupo nchini Nigeria kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka wa Afrika.

Samatta anawania tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika anayecheza ndani ya bara hilo.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment