Imegundulika kuwa shabiki mmoja wa Arsenal
alifanikiwa kumshawishi mkewe wampe mtoto wao jina la Arsenal bila mwanamke huyo
kujua.
Ikumbukwe kuwa Arsenal ni jina la timu ya soka
inayoshiriki Ligi Kuu soka nchini Uingereza na kwa sasa inaongoza katika
msimamo.
Ilikuwa ni baada ya miaka miwili ambapo mwanamke
huyo Clare Smith alijulishwa ujanja ambao mumewe alikuwa ametumia.
Bi Smith, kutoka eneo la Blacktown jimbo la New
South Wales nchini Australia, alifichua hayo kwenye barua aliyoandikia jarida
moja ambapo anasema mwenyewe hakugundua hilo hadi mumewe alipomwambia.
Amesema waliamua kumuita binti yao jina la Lanesra,
kwa sababu lilikuwa jina la kipekee na la kupendeza lakini kumbe mumewe
alitambua fika kwamba jina hilo likisomwa kutokea kulia kwenda kushoto lazima
litamkwe Arsenal.
Habari kuhusu kisa hicho zimeenezwa sana mtandaoni,
wengi wakijaribu kuandika majina ya klabu za Ligi ya Uingereza kutoka nyuma
mfano Lanesra (Arsenal) na Retseciel (Leicester)
0 comments:
Post a Comment