Timu ya soka ya Simba usiku wa leo inashuka kwenye
dimba la Amaan kucheza mchezo wake wa pili wa kundi A dhidi ya URA ya Uganda.
Mchezo huo utaanza saa 2:15 usiku ambapo Simba hadi
sasa ina pointi moja baada ya sare ya 2-2 na Jamhuri ya Pemba katika mchezo wa
kwanza huku URA ikiwa na pointi tatu baada ya juzi kuifunga JKU mabao 3-1.
Hali hiyo inailazimisha Simba ishinde mchezo wa leo
ili iweze kusonga mbele, vinginevyo safari yake itaishia hapo.
Mchezo huo utatanguliwa na mechi ya mapema ya saa 10
jioni kati ya Jamhuri na JKU.
0 comments:
Post a Comment