MBEYA CITY YAPATA KOCHA MPYA, MINGANGE APIGWA CHINI

KOCHA Kinnah Phiri aliyekuwa akikinoa kikosi cha Free State ya Afrika Kusini ametua Mbeya City na kusaini mkataba wa miaka miwili.

Katibu Mkuu wa City, Emmanuel Kimbe amethibitisha taarifa hiyo na kwamba Phiri alitua jijini Mbeya jana jioni na leo ameanza kazi huku Meja Mstaafu Abdul Mingange akipumzishwa.

Kimbe alisema kuwa moja ya kazi ambazo Phiri anatakiwa kuzifanya ni kuhakikisha anaibakisha timu kwenye ligi kwani matokeo wanayoyapata si mazuri kwao jambo analoamini kwamba litawezekana kutokana na uwezo mkubwa alionao kocha huyo.

Meja mstaafu Mingange anapumzishwa kwa matatizo ya kifamilia baada ya hivi karibuni kufiwa na mkewe.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment