England imeanza kwa kuchechemea katika mchezo wake wa kwanza wa fainali za Euro baada ya kuvutwa shati kwa sare ya 1-1 na Russia.
Mchezo huo uliochezwa usiku wa jana Jumamosi, England ilianza kupata bao kupitia kwa Dier katika dakika ya 73.
Ilionekana kama England itaibuka na ushindi lakini Russia walisawazisha katika dakika ya 90 kupitia kwa Glushakov.
Imekuwa ni kawaida kwa England kutopata ushindi katika mechi zake za kwanza za michuano hiyo kwani rekodi inaonyesha kwamba katika mechi zake za kwanza za Euro imetoka sare 5 na kupoteza mechi nne.
Katika mechi iliyotangulia hapo jana, Switzerland imejipatia ushindi wake wa pili katika michuano ya bara Ulaya baada ya kuilaza Albania 1-0.
Mapema Albania ilionekana kubabaika pale mlinda lango wao Etrit Berisha alipofanya makosa kufuatia Krosi iliopigwa na Xherdan Shaqiri na hivyobasi kuwa rahisi kwa Schar kufunga kwa kichwa.
Lakini baadaye Armando Sadiku alikosa nafasi ya wazi kabla ya nahodha wa kikosi hicho Lorik Cana kupewa kadi ya manjano kwa kuunawa mpira.
Hatahivyo kushindwa kwa Switzerland kuongeza mabao kulifanya matokeo kusalia 1-0,lakini Shkelzen Gashi karibu asawazishe kwa upande wa Albania.
Mchezaji huo wa ziada alipata pasi nzuri huku ikiwa imesalia dakika tatu lakini Kipa Yann Sommer akaupangua mkwaju wake .

0 comments:
Post a Comment