BINSLUM TYRE WANOGEWA NA MBEYA CITY FC
KAMPUNI ya Binslum Tyre ya jijini Dar es Salaam, leo imesaini mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya shilingi milioni 360 wa kuendelea kuidhamini Mbeya City FC.
Mara baada ya kusaini mkataba huo, kaimu mkurugenzi wa kampuni hiyo Mohamed Binslum alisema licha ya City kuwa na matokeo yasiyoridhishwa msimu uliopita lakini walilidhishwa kwa kiasi kikubwa namna ambavyo timu hii ilishiriki katika kuitangaza bidhaa yao na kuifikisha sehemu ilipostahili kusfika.
“City haikuwa na matokeo mazuri msimu ulipopita lakini hatuna shaka na namna walivyoitangaza bidhaa yetu, imani yetu kubwa ni kuwa mkataba huu mpya itakuwa chachu kwao ya kufanya vizuri zaidi msimu ujao” alisema.
Kwa upande wake Meya wa jiji la Mbeya, alisema kuwa anaishukuru kampuni hii kwa kuthamini mchango wa City licha ya matokeo mabaya msimu uliopita.
“Hatukuwa sawa msimu uliopita, matokeo tuliyoyapata si yale ambayo tumekuwa tukiyapata mismu miwili iliyopita, imani yangu kubwa tutafanya vizuri msimu ujao, nawashukufru Binslum kwa kutambua mchango wetu kwao, hii ni chachu kwetu kuelekea mafanikio ya msimu ujao” alisema.
0 comments:
Post a Comment