'UCHAGUZI WA MWENDOKASI' YANGA WAPATA VIONGOZI

Na Arone Mpanduka

Yusuf Manji amefanikiwa kutetea nafasi ya Uenyekiti wa Klabu ya Yanga pasi na purukushani yoyote kufuatia kukosa mpinzani kwenye nafasi hiyo.

Clement Sanga nae ametetea nafasi ya Makamu Mwenyekiti kwa kumbwaga mpinzani wake Titus Osoro.

Shughuli pevu ilikuwa kwa wagombea nafasi ya ujumbe ambapo jumla ya wagombea 20 walikuwa wakiwania nafasi 8 za ujumbe.

KURA WALIZOJIZOLEA
Kwa mujibu wa matokeo yaliyotolewa na  kamati ya uchaguzi ya Yanga,Manji ameibuka mshindi wa nafasi ya Uenyekiti bila kupingwa na kupata idadi ya kura 1468 zilizopigwa na wanachama, huku kura 2 pekee zikiwa zimeharibika.

Clement Sanga amemgaragaza mpinzani wake baada ya kupata kura 1428 wakati mpinzani wake Titus Osoro akiambulia kura 80 pekee.

WAJUMBE WALIOSHINDA
Omary S. Amei(kura 1069), Siza Lyimo(kura 1027), Salum Mkemi(894), Tobias Lingalangala(889), Ayoub Nyenzi(889) Samwel Lukumay(818), Hussein Nyika(770)na Hashim Abdallah(727).

SAFU KAMILI YA UONGOZI
uongozi mpya wa Yanga uliochaguliwa na wanachama unaundwa na Mwenyekiti Yusuf Manji, Makamu Mwenyekiti Clement Sanga huku wajumbe wakiwa ni Omary S. Amei, Siza Lyimo, Salim Mkemi, Tobias Lingalangala, Ayoub Nyenzi, Samwel Lukumay, Hussein Nyika na Hashim Abdallah

UCHAGUZI WA MWENDOKASI
Uchaguzi huo waweza kuuita wa mwendokasi kufuatia mchakato wake kwenda haraka tangu ratiba ilipotangazwa Juni mosi mwaka huu.

Mchakato wa uchaguzi huo umechukua takribani siku kumi tu kukamilika ikiwa ni tofauti na chaguzi zingine zilizopita ambazo matukio yake yalichukua siku nyingi.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment