Yahya Mohamed (kulia)akizungumza na waandishi wa habari asubuhi ya leo (Picha kwa hisani ya TFF) |
Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Yahya
Mohamed leo amefungua semina ya mafunzo ya leseni za klabu kwenye Ukumbi wa Mikutano
wa Dar es Salaam International Conference Centre (DICC) uliopo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi
wa semina hiyo, Yahya amesema imekua jambo jema kwa CAF kutupatia nafasi ya
mafunzo ya leseni za klabu hapa nyumbani, kwani viongozi wa klabu wote wanapata
nafasi ya kushiriki semina hii ya siku mbili kutoka kwa wakufunzui wa CAF.
“Uendeshaji wa mpira wa miguu duniani umebadilika,
mabadiliko haya yapo katika nyanja zote za uongozi (utawala), miundombinu, kitu
ambacho kwa sisi Tanania tumeshaanza kuendana na mabadiliko hayo, na sasa
kupata kwetu semina hii kutawafanya viongozi wengi kufahamu umuhimu wa leseni
za vilabu na kufanyia kazi mapungufu yaliyokuwepo” alisema Yahya.
Semina hiyo ya Leseni za klabu itakayofanyika kwa siku
mbili inaedeshwa na wakufunzi watatu kutoka CAF ambao ni Dk Bolaji Ojo Oba
(Nigeria), Amanze Uchegbulanm (Nigeria) na Othman Mohamed kutoka nchini Sudan.
Agizo la CAF ni kuwa kila klabu inayoshiriki michuano
ya kimataifa (Ligi ya Mabingwa, Kombe la Shirikisho) lazima iwe imepata leseni
hiyo ambayo itaipa nafasi ya kushiriki michuano inayoandaliwa na CAF, na kwa klabu
ambayo haitatimiza mahitaji ya kupata leseni hiyo haitaweza kushiriki michuano
ya kimataifa.
Ili kupata leseni ya klabu, klabu inapaswa kutimiza
vigezo vilvyowekwa ikiwemo masuala ya utawala, ripoti ya mapato na matumizi
iliyokaguliwa, uwanja wa mazoezi nk.
Mmiliki mmoja wa klabu hatarusiwa kumiliki timu zaidi ya moja kwenye ligi moja, kila klabu lazima iwe na program za vijana na uwanja wa mazoezi.
TAARIFA IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU NCHINI TFF
0 comments:
Post a Comment