Kundi la wanariadha waliojawa na hasira limevamia
makao makuu ya shirikisho la riadha nchini Kenya AK na kufunga milango
wakilalamikia ubadhirifu na ufisadi katika jumba la Riadha mjini Nairobi.
Wanariadha hao waliwazuia maafisa wa shirikisho hilo
la AK kuingia ofisini mwao.
Walikuwa wamebeba mabango ya kukashifu uongozi duni
na ufisadi uliokithiri ofisini humo.
Maandamano hayo yanafuatia madai ya hivi karibuni kuwa
takribani dola laki saba na nusu za Marekani ambazo ni za ustawishaji wa riadha
nchini Kenya zililiwa na maafisa wakuu watatu wa shirikisho hilo.
Fedha hizo zilikuwa zimetolewa na kampuni ya
kutengeneza bidhaa za michezo Nike.
Naibu mwenyekiti wa shirikisho hilo David Okeyo
tayari anachunguzwa na idara ya kupambana na ufisadi.
Lakini Okeyo amekana madai hayo dhidi yake.
Vilevile wanariadha hao wanailaumu shirikisho hilo
la Atheltics Kenya kwa kupokea hongo kutoka kwa mawakala wanaoshukiwa
kuwashawishi wanariadha nchini humo kutumia madawa ya kutitimua misuli
yaliyopigwa marufuku duniani.
Kenya ni moja ya mataifa yaliyotajwa kuwa na tatizo
sugu la utumiaji wa dawa hizo za kuongeza nguvu mwilini na shirikisho la
kupamabana na matumizi ya dawa hizo duniani WADA.
0 comments:
Post a Comment