Klabu ya Corinthians wametawadhwa
mabingwa wapya wa Brazil jana baada ya sare ya bao 1-1 waliyopata dhidi ya
Vasco da Gama na kusaidiwa na kipigo cha mabao 4-2 walichpata Atletico Mineiro
dhidi ya Sao Paulo ambacho kimewafanya kuongoza kwa alama 12 huku zikiw
zimesalia mechi tatu.
Corinthians ndio vinara wa mabao
katika ligi na safu imara ya ulinzi huku pia wakiwa wameshinda mechi nyingi
zaidi na kufungwa chache kuliko timu nyingine yeyote.
Klabu hiyo hiyo imenyakuwa taji hilo
ambalo ni la sita kwao wakiwa wanaongoza kwa alama 77 wakati Atletico waliokuwa
wakifuatia wakiwa na alama 65.
Akihojiwa golikipa wa Corinthians
aliwapongeza wachezaji wenzake kwa jinsi walivyojituma na kuongeza kuwa
walistahili taji hilo.
0 comments:
Post a Comment