Filamu ya mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano
Ronaldo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi Novemba 9 mwaka huu na kuonyeshwa kwenye
majumba mbalimbali ya sinema duniani.
Moja kati ya vipande vya filamu hiyo vinamuonesha
mama wa Ronaldo Maria Dolores dos Santos Aveiro akiweka wazi kuwa alitaka kutoa
ujauzito wa Ronaldo.
Akinukuliwa katika kipande hicho mama wa Ronaldo
anasema “nilitaka kutoa ujauzito wa Ronaldo lakini Mungu hakutaka iwe hivyo.
Ronaldo hakuwa akihitajika kwangu kwa sababu
nilitaka kuutoa ujauzito wake lakini mpaka sasa amenifanyia mambo makubwa”
anamalizia mama wa Ronaldo Maria Dos Santos.
Filamu hiyo itakuwa na vipande mbalimbali vikielezea
maisha ya Ronaldo pamoja na familia yake na imemchukua miezi 14 kutengeneza
filamu hiyo.
Pia filamu ya Ronaldo itamzungumzia baba yake
Ronaldo anayefahamika kama José Dinis Aveiro.
Baba yake Ronaldo alikuwa akifanya kazi ya kutunza
bustani katika manispaa ya Funchal katika mji wa Medeira nchini Ureno lakini
alikuwa ni mlevi sana.
0 comments:
Post a Comment