Na Arone Mpanduka
Tanzania imeendelea kupaa katika viwango vya ubora
vya Shirikisho la soka Duniani FIFA baada ya kupanda kwa nafasi moja zaidi.
Kwa mujibu wa tovuti ya FIFA, Tanzania imeshika
nafasi ya 135 duniani kwa mwezi Oktoba kutoka katika nafasi ya 136 iliyoshika
kwa mwezi Septemba.
Kwa ujumla Tanzania imeweza kupanda kwa nafasi 5
ndani ya miezi miwili ambapo kwa viwango vya mwezi Septemba ilipanda kwa nafasi
nne na kushika nafasi ya 136 kutoka 140.
Nafasi hiyo inachagizwa na matokeo ya kuridhisha ya
timu ya Taifa Stars kwa mechi za mwezi Oktoba ambapo ilicheza mechi mbili dhidi
ya timu ya Taifa ya Malawi na kufanikiwa kuitupa nje ya kinyang’anyiro cha
kuwania kufuzu fainali za Afrika.
Mchezo wa kwanza Stars iliifunga Malawi 2-0 kwenye
uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na kisha kupokea kichapo cha bao 1-0
ugenini na kusonga mbele kwa mabao ya jumla ya 2-1.
Ili iweze kupaa tena kwa viwango vya mwezi huu, Taifa
Stars inapaswa kufanya vizuri kwenye mechi za kuwania kupangwa kwenye makundi
ya kusaka tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwaka
2018 nchini Uswis.
Mechi hizo ni zile dhidi ya Algeria ambapo moja
itakuwa nyumbani na ya marudiano itachezwa ugenini.
0 comments:
Post a Comment