HOFU YA BOMU YASABABISHA POLISI KUITOA HOTELINI TIMU YA UJERUMANI
Polisi wamelazimika kuwatoa wachezaji wa timu ya taifa Ujerumani mjini Paris, Ufaransa baada ya kuwepo kwa taarifa ya bomu.
Taarifa hizo zilitolewa na mtu mmoja aliyejiita raia mwema akidai kuna bomu eneo hilo.
Ilikuwa ni saa 3:50 asubuhi, Polisi wa Ufaransa walipolazimika kufika hotelini hapo na kuwaondoa wachezaji hao wa timu ya taifa ya Ujerumani walio mjini hapo kujiandaa na mechi yao kirafiki dhidi ya wenyeji Ufaransa, leo.
Hata hivyo uchunguzi wa mwisho wa polisi baadaye ulibaini eneo hilo lilikuwa salama.
0 comments:
Post a Comment