'MADADA' KUZICHAPA KESHO MWANANYAMALA
Mabondia Asha Nzowa na Joyce Awino asubuhi ya leo wamepima uzito kwa ajili ya pambano la kesho lisilo na ubingwa litakalofanyika kwenye ukumbi wa CCM Mwinjuma, Mwananyamala jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mratibu wa pambano hilo ambaye pia ni kocha wa masumbwi,Mhamila Rajab, maandalizi yote yapo vizuri.
Amesema lengo la pambano hilo ni kutanua wigo wa masumbwi kwa wanawake ambao wengi wamekuwa wakiogopa.
0 comments:
Post a Comment