KOMBE LA DUNIA LAZUA MIMBA NYINGI














Mashindano ya kombe la dunia ya mwaka 2010 nchini Afrika Kusini, yalichochea ongezeko la idadi ya watoto wa kiume waliozaliwa nchini humo, miezi tisa baada ya mashindano hayo kuanza.




Kwa mjibu wa taarifa iliyochapishwa katika jarida la Early Human Development.

Kiwango cha wavulana waliozaliwa katika kipindi hicho kilikuwa kikubwa mno kati ya miaka 2003 na 2014.

Inasemekana kuwa kutokana na mchuano huo wa kombe la dunia wanaume wengi walibaki makwao na hivyo kuchochea kufufuka kwa ndoa zilizokuwa zimefifia.

''watu walikuwa watulivu zaidi, na kuna uwezekano walijihusisha katika tendo la ndoa zaidi wakati wa mashindano hayo ya kombe la dunia, hali iliyofanya ongezeko kubwa ya idadi ya wanawake waliopata ujauzito.'' Watafiti wamesema.

Watoto wengi walizaliwa miezi tisa baada ya kombe la dunia

Afrika Kusini iliandaa mashindano hayo ya kwanza kabisa barani Afrika kati ya Juni 11 hadi Julai 11 2010.

'HISIA NZURI'

Dkt Gwinyai Masukume, kutoka Chuo kikuu cha Witwatersrand, alikuwa miongoni mwa waliofanya utafiti huo na akaiambia idhaa ya BBC kuwa

"kombe la dunia liliwafanya watu kutulia mno kiakili, walikuwa na hisia nzuri mno, wakijiwazia mema na pia kufurahia taifa lao.''

"Watu pia walijamiania kupita kiasi wakati wote wa michuano ya kombe la dunia."

Idadi ya watoto wa kiume waliozaliwa yapata miezi tisa baada ya mashindano ya kombe la dunia ilikuwa asilimia 0.5063, zaidi ya watoto wa kike.

Idadi ya watoto wa kiume waliozaliwa yapata miezi tisa baada ya mashindano ya kombe la dunia ilikuwa asilimia 0.5063, zaidi ya watoto wa kike.

Hii iliashiria watoto wa kiume waliazaliwa takriban 1,088 mwaka uliopfatwa ikilinganishwa na miaka ya awali.

Kisa na maana ''wanaume walishiriki ngono kupita kiasi,kuimarika kwa afya ya manii na kupungua kwa idadi ya watoto wa kiume waliokufa punde baada ya kuzaliwa.

MAKALA HAYA NI KWA MUJIBU WA TOVUTI YA BBC
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment