Kikosi cha Taifa Stars wakati kikifanya mazoezi jioni ya leo |
Na Arone Mpanduka
Watu wasiofahamika wenye asili ya kiarabu jioni ya
leo wametimuliwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam baada ya kutaka
kurekodi mazoezi ya timu ya Taifa Stars bila ridhaa ya benchi la ufundi.
Kikosi cha Taifa Stars jioni ya leo kilifanya
mazoezi kwenye uwanja wa Taifa kwa lengo la kujiweka sawa kuelekea kwenye
mchezo wa keshokutwa wa kusaka tiketi ya kushiriki fainali za kombe la dunia
dhidi ya Algeria.
Akizungumza na mpanduka.blogspot.com, Meneja wa Taifa
Stars Omary Kapilima alisema wanahisi kwamba waarabu hao ni watu wa karibu na
timu ya taifa ya Algeria ambao nia yao ilikuwa ni kuzipeleleza mbinu za timu
hiyo kabla ya mchezo.
Kapilima alisema baada ya sura hizo za kiarabu
kuonekana uwanjani ilibidi mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la soka
nchini TFF ambaye pia ni mmoja wa wanakamati ya Taifa Stars, Ahmed Msafiri
Mgoyi kuwatimua na kuwataka wakae nje ya eneo la uwanja.
Alisema waarabu hao walitakiwa kukaa nje ya uwanja
hadi mwisho wa mazoezi ndipo wafanye mahojiano na wachezaji wa Taifa Stars.
"Hatuna uhakika sana kama waarabu hao ni waandishi wa habari ama la kwa sababu walikuja na kamera zao na kutaka kurekodi mazoezi ya timu yetu lakini Mgoyi akawazuia kufanya hivyo," alisema Kapilima.
"Tutaendelea kuwa makini katika muda huu uliobaki ili tusiruhusu ujanja wowote kutoka kwa wapinzani wetu"
0 comments:
Post a Comment