Aliyekuwa kocha msaidizi wa klabu ya Simba SC
Selemani Matola, leo amesaini mkataba wa mwaka mmoja na timu ya Geita Gold FC
inayoshiriki ligi daraja la kwanza Tanzania bara.
Novemba 11 mwaka huu, Matola aliandika barua kwa
ajili ya kuomba kujiuzulu ndani ya Simba kwa madai kuwa hana maelewano mazuri
na kocha mkuu Dylan Kerr.
Matola amekuwa kocha msaidizi kwenye kikosi cha
Simba kwa muda mrefu baada ya kuitumikia Simba kama mchezaji na nahodha pia.
Geita Gold FC ipo kundi C na inafanya vizuri kwenye
kundi hilo ikiwa inachuana kwa karibu na JKT Olijoro inayoongoza kundi hilo
ikiwa na kileleni kwa pointi 14.
Kwenye kundi C kuna timu za Geita Gold FC, JKT
Oljoro, Polisi Tabora, Panone FC, Mbao FC, Rhino Rangers, Polisi Mara na JKT
Kanembwa.
Baada ya kutua kwenye kikosi hicho Matola atakuwa na
kazi ya kuhakikisha anakisaidia kupanda daraja kwa ajili ya kushiriki ligi kuu
ya Vodacom Tanzania bara.
0 comments:
Post a Comment