MTIBWA SUGAR YAANZA 'MATIZI'

Na Arone Mpanduka

Timu ya soka ya Mtibwa Sugar ya Morogoro imeanza mazoezi kujiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara.

Ligi hiyo imesimama kwa muda tangu mwisho wa mwezi uliopita na itaendelea tena mwanzoni mwa mwezi ujao.

Lengo la Shirikisho la soka nchini TFF kusimamisha ligi hiyo ni kupisha mechi za kimataifa za timu ya taifa, Taifa Stars pamoja na Kilimanjaro Stars ambayo kwa sasa ipo nchini Ethiopia kushiriki michuano ya Chalenji.

Akizungumza na mpanduka.blogspot.com msemaji wa Mtibwa Sugar Thobias Kifaru alisema wameamua kuanza mazoezi na watakuwa wakijifua ufukweni jijini Dar es salaam na kisha kurejea tena nyumbani Morogoro.

"Tumeamua kuanza mazoezi kwa kuwa hatuna wachezaji wengi wanaocheza katika timu za Taifa,"alisema Kifaru.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment