Na Arone Mpanduka
Klabu ya soka ya Yanga imesema haina mpango wowote
wa kuongeza mchezaji katika kipindi cha sasa cha dirisha dogo la usajili.
Akizungumza na mpanduka.blogspot.com jioni ya leo, Katibu
mkuu wa klabu hiyo Dokta Jonas Tiboroha alisema kikosi chao kimekamilika hivyo
hawaoni haja ya kuongeza wachezaji wengine.
Alisema programu ya kocha Hans van Der Pluijm haimpi
nafasi ya kuongeza wachezaji wengine labda itokee dharura ya namna yoyote
itakayomlazimu kubadili maamuzi yake.
“Kwa kikosi tulichonacho sidhani kama kuna ulazima
wa kuongeza mchezaji yeyote.Halafu kipindi hiki ni kigumu sana kupata mchezaji
kwa sababu kila mchezaji unakuta ana mkataba mrefu sana,” alisema Tiboroha
Kipindi cha dirisha dogo la usajili ambacho kilianza
Novemba 15 mwaka huu kitafikia tamati Desemba 15 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment